Ditutup

ARUSI YA MZOFAFA

Majina yangu ni Melvin Jeudi. Asili yangu ni Kenya. Filihali ninaishi katika jiji kuu la Nairobi. Kazi na bazi yangu ni uandishi wa makala anuwai kuhusu kiswahili. Kwa yakini bali si kwa yamkini nimebobea na kutopea katika Kiswahili. Ari na azima yangu ni kutoa huduma zangu za uandishi kwa kila awaye na haja ya huduma zangu.

Usiku wote sikupata hata lepe la usingizi. Niliwaza na kuwazua namna siku ambayo ilifuata ingekuwa kwangu mimi baada ya kuisuburi kwa pashau kubwa. Hatimaye kulikucha jua likapasua matlai na kudhihirisha wazi kuwa, waswahili hawakukata bugi waliposema kuwa, hakuna kubwa lisilo ukomo.

Saa tatu zilifika mimi na wapambe wangu tukiwa tayari tumejikwatua kama malkia. Mimi binafsi nilivaa veli nyeupe kama joya pamoja na mapambo yenye widadi. Nywele zangu za singa na nyeusi kama masizi, nilizipiga kitana zikashirikiana na uso wangu wa haiba na haya, kunifanya mrembo wa kani mwenye ulimbo. Kama ilivyo desturi ya kila bibi arusi, nilikifunika kichwa na uso wangu kwa ushungi ulioenda urari na veli.

Saa moja baadaye msafara wa magari yangu ulifika kanisani. Pindi tu tulipoingia uani tulilakiwa kwa hoihoi ya arusi. Wanawake wenye nyuso zenye furaha kama mapambazuko, walitangaza kufika kwetu kwa shangwe na hoihoi. Kwa mara ya kwanza moyo wangu ulipata utulivu japo kwa sekunde kadhaa. Tulilazimika kubaki magarini mwetu kwa kipindi cha robo saa. Huu ulikuwa wakati ambapo mfawidhi wa arusi yangu, alikuwa akiwaomba watu wote kwa udhu na adabu kuingia ndani ya kanisa. Kulingana na utaratibu uliotiwa, nilifaa kuwa mtu wa mwisho kuingia kanisani. Kwa yakini bali si kwa yamkini, siku hiyo hadhi yangu ilikuwa zaidi ya hadhi ya binti Huzaima.

Hatimaye ulifika muda wa kungia kanisani. Mwanzo wapambe wangu waliingia kwa mwendo wa dalji, uliolingana na midundo ya nyimbo zilizoimbwa, bila haraka yoyote. Si siri kuwa walijua kuwa maneno ya wakale, haraka haraka haina baraka, si maneno ya mporoto. Baada yao kuwatangazia waumini mjo wangu, nilitoka garini mwangu kwa madaha na madahiro. Kama kinyonga, nilikanyaga kwa mwendo wa tao kuelekea kanisani. Nilipofika mlangoni nilishangiliwa kwa namna zote. Sauti za vifijo, mbinja, makofi, filimbi, matari na kuro zilisikika hadi nilipokaa raha mustarehe. Pale kitini pangu nilipogea macho, nilibaini kuwa kanisa zima lilikuwa limejaa chekwa. Hapo nikajua kuwa nilikuwa mtoto wa watu aliyependwa kama kito.

Baada ya mahubiri mafupi, ulifika wakati uliosubiriwa na kila mmoja kwa hamu na ghamu. Huu ulikuwa wakati wa maarusi kutoleana lulu, kuvishana pete na kupigana kisi. Hilo la kupigana kisi kadamnasi liliufanya moyo wangu kudunda kama saa kweche mezani. Bwana arusi alipoitwa mbele, macho yangu yalifurahi na moyo wangu kumriadhia. Kwa hakika alikuwa matlai shamsi wa kiume. Baada yake niliitwa kisha kasisi akamwamuru kuiondoa veli kwenye uso wangu. Alipofanya vile alikaa kinywa wazi kwa sekunde kadhaa kutokana na urembo wangu. Lililofuata lilikuwa kulishana kiapo, kuvishana pete. Kisha bwana arusi aliagizwa kunibusu. Lisilobudi hutendwa. Nililazimika kufumba macho na kupigwa busu shingo mkingamo.

Hatimaye tulielekea kwenye bustani kupigwa picha kwa ajili ya kumbukizi ya siku hiyo ya kiu kubwa. Kilele cha arusi hiyo kilikuwa katika hoteli ya Miloyetu. Hii haikuwa hoteli ya akina yahe ila siku hii waliruhusiwa kuingia ndani kwa sababu ya arusi yangu. Hotelini mle kila mtu alikula shibe yake. Baada ya kula, tulipokezwa zawadi chungu nzima. Huku tukipokezwa zawadi, muziki wa taarabu uliimba watu wakacheza densi ya kuvunja jungu.

Mwendo wa saa kumi na mbili jioni, tulianua majamvi kwa kugongeana bilauri na jamaa na marafiki kisha tukaenda zetu Dar-es-salaam kwa ajili ya fungate.

Kemahiran: Penulisan Semula Artikel, Penulisan Kreatif, Storyboard

Lihat lagi: hadi hammam, cataln vasco gallego ya tienen traductor online, desde ya gracias traduccionb advance, fix ya php clone, ghostwrite childrens ya literature, make ya chat room paltalk, necesito una carta en ingles ya hecha maximo de palbras, remove forum ya com, type ya writes, hadi ghoghai, hadi puspa handoyo batam, mohit hadi, abdul hadi lane dhaka 1000, ipung hadi purjono, freelance ya editor wanted, hadi saleh, hadi, mi proyecto es una pagina web que tiene suscriptores gratis y pagos ya tengo una pagina, YA, il ya une platforme de freelenceur developpeur ivoirienn

Tentang Majikan:
( 0 ulasan ) Nairobi, Kenya

ID Projek: #25186784

7 pekerja bebas membida secara purata $19/jam untuk pekerjaan ini

henricamonayo

pokea salamu Ningependa sana kukusaidia katika kuikamilisha kazi yako ijapokua sijafahamu vema unalotaka kufanyiwa , hata hivyo ningependa kukuhakikishia kua nina ujuzi katika ubunifu wa hadithi na uandishi mbali Lagi

$16 USD / jam
(0 Ulasan)
0.0
Jaredngere

Hujambo, Heko kwa kazi bora nimeona umejizatiti kuandika. Tafadhali toa maelezo kamili ya yale unayotaka utekelezewe, Nina uzoefu Katika lugha Ya kIswahili na Kiingereza Tunaweza wasiliana kwa 'chat' iliunipe maagizo z Lagi

$16 USD / jam
(0 Ulasan)
0.0
$22 USD / jam
(0 Ulasan)
0.0
githigajoyce515

Hujambo bwana Melvin. Natumai u buheri wa afya. Mimi si mchache ila nina machache. Ndoto yangu ya kuja kuandika kitabu itakua imetimia kupitia kushirikiana nawe. Nichague tuchanganue. Asante. Relevant Skills and Exper Lagi

$28 USD / jam
(0 Ulasan)
0.0
Asambre

hujambo dada jina langu ni Enock Asamba kutoka maeneo ya nyanza. niko tayari kuifanya kazi yako. kuja inbox tuongee kwa upana

$15 USD / jam
(0 Ulasan)
0.0
Musaah

Ninakusihi ya kwamba jicho lako liweze kuelekezwa kwa sanaa yangu niloyobobea

$18 USD / jam
(0 Ulasan)
0.0
carolynekimani96

This may be useful in teaching Kiswahili learners creative writing. Since there is need for creative writing among all people, there is need to provoke our mind and create a society that can create.

$15 USD / jam
(0 Ulasan)
0.0